Kumb.Na.JA.9/259/01/B/120
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs anapendakuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanziatarehe 17-01-2025 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.Wasailiwawanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
1. Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapousaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
2. Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
3. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
4. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua yautambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
5. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI,Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, ada na kuendelea kutegemeana na sifa zaMwombaji. 6. Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatizamatokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NAHAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI. 7. Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
8. Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili.
9. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa naMamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
10. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhivigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji yatangazo husika.
11. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyetivyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
12. Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili nambaya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
Contents
- 1 WALIOITWA KWENYE USAILI KADA ZA UALIMU MIKOA YA KILIMANJARO,LINDI,MANYARA,MARA,MBEYA NA MOROGORO 11-01-2025
- 2 WALIOITWA KWENYE USAILI KADA ZA UALIMU MIKOA YA GEITA,IRINGA,KAGERA,KATAVI NA KIGOMA 11-01-2025
- 3 WALIOITWA KWENYE USAILI MIKOA YA ARUSHA,DAR ES SALAAM NA DODOMA 11-01-2025
- 4 WALIOITWA KWENYE USAILI KADA ZA UALIMU MIKOA YA SIMIYU, SINGIDA, SONGWE, TABORA, TANGA NA ZANZIBAR 11-01-2025
- 5 WALIOITWA KWENYE USAILI MTWARA, MWANZA, NJOMBE, PWANI,RUKWA, RUVUMA SHINYANGA 11-01-2025
WALIOITWA KWENYE USAILI KADA ZA UALIMU MIKOA YA KILIMANJARO,LINDI,MANYARA,MARA,MBEYA NA MOROGORO 11-01-2025
MAJINA YA WASAILIWA WA KADA ZA UALIMU WATAKAOFANYIA USAILI MKOA WA KILIMANJARO
KWA WENYE USAILI WA KUANDIKA USAILI HUO UTAFANYIKA: CHUO CHA USHIRIKA MOSHI (MOCU)
USAILI WA MAHOJIANO UTAFANYIKA: CHUO CHA USHIRIKA MOSHI (MOCU)
WALIOITWA KWENYE USAILI KADA ZA UALIMU MIKOA YA GEITA,IRINGA,KAGERA,KATAVI NA KIGOMA 11-01-2025
MAJINA YA WASAILIWA WA KADA ZA UALIMU WATAKAOFANYIA USAILI MKOA WA GEITA
KWA WENYE USAILI WA KUANDIKA USAILI
- SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA NYANKUMBU
- SHULE YA SEKONDARI MWATULOLE
USAILI WA MAHOJIANO UTAFANYIKA: SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA NYANKUMBU
WALIOITWA KWENYE USAILI MIKOA YA ARUSHA,DAR ES SALAAM NA DODOMA 11-01-2025
MAJINA YA WASAILIWA WA KADA ZA UALIMU WATAKAOFANYIA USAILI MKOA WA ARUSHA
KWA WENYE USAILI WA KUANDIKA USAILI HUO UTAFANYIKA: CHUO CHA UHASIBU ARUSHA (IAA)
USAILI WA MAHOJIANO UTAFANYIKA: CHUO CHA UHASIBU ARUSHA (IAA)
WALIOITWA KWENYE USAILI KADA ZA UALIMU MIKOA YA SIMIYU, SINGIDA, SONGWE, TABORA, TANGA NA ZANZIBAR 11-01-2025
MAJINA YA WASAILIWA WA KADA ZA UALIMU WATAKAOFANYIA USAILI MKOA WA SIMIYU
KWA WENYE USAILI WA KUANDIKA USAILI HUO
UTAFANYIKA: SHULE YA SEKONDARI BARIADI, KUSEKWA MEMORIAL SEKONDARY SCHOOL
USAILI WA MAHOJIANO UTAFANYIKA: SHULE YA SEKONDARI SIMIYU
WALIOITWA KWENYE USAILI MTWARA, MWANZA, NJOMBE, PWANI,RUKWA, RUVUMA SHINYANGA 11-01-2025
MAJINA YA WASAILIWA WA KADA ZA UALIMU WATAKAOFANYIA USAILI MKOA WA MTWARA
KWA WENYE USAILI WA KUANDIKA USAILI HUO UTAFANYIKA: TANZANIA INSTITUTE OF ACCOUNTANCY- MTWARA CAMPUS
USAILI WA MAHOJIANO UTAFANYIKA: CHUO CHA UALIMU UFUNDI – MTWARA