Kampuni ni nini?
Kampuni ni mjumuiko wa watu wawili au zaidi wenye nia ya kufanya biashara halali na kuusajili mjumuiko huo chini ya Sheria ya kampuni.
Aina za Kampuni
- Kampuni ya kigeni
- Kampuni binafsi
- Kampuni ya umma
Faida za Urasimishaji Kampuni ni zipi?
- Kuipatia utu wa kisheria biashara yako
- Kutambulika na taasisi za fedha mf. benki wakati wa kufungua akaunti.
- Kupata mikopo katika taasisi za fedha kama benki.
- Kupanua wigo wa kufanya biashara kubwa, mf. biashara za kimataifa
- Urahisi wa kuitangaza kampuni kwa urahisi na kupanua wigo wa wateja.
Vigezo vya kusajili Kampuni
- Mwombaji anatakiwa kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA
- Namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA ya kila mwanahisa
- Namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA au pasi ya kusafiria kwa raia wa kigeni na namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN) ya kila mkurugenzi
Nyaraka za kuambatisha
- Katiba ya Kampuni
- Fomu ya uadilifu
- Fomu ya majumuisho (Consolidated Form)
Hatua 10 za kusajili Kampuni
- Tembelea “www.brela.go.tz” au “ors.brela.go.tz“.
- Ingia katika akaunti yako ya Usajili kwa njia ya mtandao (ORS) au tengeneza akaunti katika mfumo.
- Chagua “huduma mtandao”.
- Chagua “kampuni”.
- Chagua “aina ya huduma”.
- Chagua “aina ya kampuni”.
- Jaza taarifa za kampuni husika.
- Pakia viambatisho katika mfumo.
- Lipa kwa njia ya simu au benki.
- Maombi yatafanyiwa kazi baada ya malipo kupokewa.